Banka kuuwahi mchezo dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2019
Banka kuuwahi mchezo dhidi ya Simba

Kiungo Mohammed Issa 'Banka' tayari ameanza kujifua na kikosi cha Yanga akitarajiwa kuanza kuonekana rasmi dimbani Februari 08 2019

Banka huenda akaichezea Yanga kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa dimba la Mkwakwani, Februari 09 2019

Kiungo huyo mwenye 'mapafu ya Mbwa' atauwahi mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba utakaopigwa Februari 16 katika dimba la Taifa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Banka ataongeza nguvu na kasi ya mashambulizi Yanga.

Amesema licha ya kutocheza kwa zaidi ya miezi 10, Banka anaonyesha uwezo mkubwa mazoezini huku akionekana 'yuko fit'

Ujio wa Banka ni habari nzuri kwa Yanga ambayo haikufanya usajili mkubwa wakati wa dirisha dogo kutokana na changamoto za kiuchumi

Banka atakuwa kama usajili mpya. Yanga iliwasajili Haruna Moshi 'Boban' na Ibrahim Hamid pekee.

Mwenyewe amesema anasubiri kwa hamu kuanza kuitumikia Yanga iliyomsajili kutoka klabu ya Mtibwa Sugar

Amesema atashirikiana na wachezaji waliopo kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’