Kakolanya agoma kuzungumzia hatma yake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2019
Kakolanya agoma kuzungumzia hatma yake Yanga

Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya amesema amemwachia Mwanasheria wake kumalizana na timu hiyo kuhusu ajira yake

Kumekuwa na shauku kubwa miongoni mwa mashabiki wa Yanga ambao wengi wangependa kumuona Beno akiendelea na majukumu yake katika klabu hiyo

Juhudi zimekuwa zikifanyika kumaliza tofauti iliyojitokeza baina yake na mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutomuhitaji

Hata hivyo Kakolanya nae amevunja ukimya kwa kusema hatma yake ameiacha mikononi mwa Mwanasheria wake ambaye tayari amekutana na uongozi wa Yanga mara kadhaa

"Siwezi kuongelea lolote kuhusu ajira yangu maana hilo swala nilishamkabidhi Mwanasheria wangu analishughulikia, nipo kimya sitaki kuliongelea ila hivi karibuni atawataarifu nini hatma ya swala hili," amesema Beno

Ingawa hakuweka wazi nini kinashughulikiwa na Mwanasheria huyo, lakini inafahamika uongozi wa Beno uliiandikia barua klabu ya Yanga ukiomba kuvunjwa kwa mkataba wake

Barua hiyo iliandikwa wakati Beno alipogoma kushinikiza alipwe stahiki zake.

Mwanasheria wa Beno ameweka msisitizo wa kuitaka klabu ya Yanga imuachie mteja wake kwa kuwa ameendelea kukaa nje hali inayohatarisha kipaji chake

Huenda uongozi wa Yanga ukalazimika kufanya maamuzi haraka au jambo hilo litaenda kumalizwa Mahakamani

Wakati huo huo baadhi ya wadau wameitaka klabu ya Yanga ifanye uamuzi ili kuepuka makundi yaliyoanza kujitokeza miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo

Lipo kundi linalomuunga mkono Kocha Mwinyi Zahera kwa uamuzi wake wa kukataa kumrejesha Beno kikosini baada ya kuchukizwa na utaratibu alioutumia kujiondoa , wakati kundi la pili linapingana na uamuzi huo wakishinikiza mlinda lango huyo arejeshwe kutokana na kutoridhishwa na viwango vya walinda lango waliopo

Uongozi wa Yanga umetakiwa uamue moja ili kumaliza sintofahamu hiyo ambayo imeanza kuutafuna umoja uliopo

Aidha wapo wasioitakia mema Yanga ambao pia wanatumia mgogoro huo kuwachochea WanaYanga ili wamchukie kocha wao Mwinyi Zahera hali ambayo itaigharimu timu hiyo zaidi iwapo kocha huyo ataamua kuondoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’