Yanga kamili kuikabili Stand United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2019
Yanga kamili kuikabili Stand United

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wako mkoani Shinyanga ambapo leo wanashuka katika dimba la Kambarage kuikabili Stand United

Yanga inayoshikilia rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi msimu huu, itakuwa ikisaka alama tatu muhimu ili iendelee kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambao Yanga iliifunga Stand mabao 4-3

Katika mchezo huo Stand United ilionyesha upinzani mkali kwa Yanga na itataka kuendeleza pale ilipoishia na hasa ikizingatiwa itakuwa ikicheza katika dimba lake la nyumbani

Zahera amesema amewaagiza vijana wake kuhakikisha wanajituma ili kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo

Mchezo utapigwa saa kumi kamili jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’