Zahera asisitiza, Makambo bado yupo sana Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jan 2019
Zahera asisitiza, Makambo bado yupo sana Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mshambuliaji wa timu hiyo kinara wa mabao Heritier Makambo alipewa ruhusa kwenda nchini Congo na atarudi

Baada ya kuibuka kwa taarifa hapo jana kuwa mshambuliaji huyo alitoroka kambini, Zahera amesema taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote kwani Makambo aliondoka baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City

"Baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City tuliwapa wachezaji wote mapumziko. Makambo aliondoka siku moja baada ya mchezo huo," Zahera amewaambia waandishi wa habari

Mimi na Kindoki tuna namba ya Makambo, tunawasiliana nae atarejea kuna mambo alikuwa anaweka sawa"

Makambo mwenye mabao 11 amekosa mchezo dhidi ya Mwadui Fc leo lakini licha ya kukosekana kwake Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1

Pacha wake Amissi Tambwe amefunga moja ya mabao hayo na kumfanya afikishe mabao sita na kuweka hai ndoto ya kuwawania kiatu cha dhahabu msimu

Makambo anatarajiwa kuuwahi mchezo wa ugenini dhidi ya Stand United utakaopigwa Jumamosi, Januari 19 dimba la Kambarage mkoani Shinyanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’