Makambo amepatikana, kutua wakati wowote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jan 2019
Makambo amepatikana, kutua wakati wowote

Uongozi wa Yanga umetoa taarifa njema kwa mashabiki wake kuwa mshambuliaji Heritier Makambo amepatikana na yuko njiani kurejea nchini.

Jana zilitolewa taarifa za mkanganyiko kuhusu mshambuliaji huyo ambaye alikuwa hapatikani kwenye simu kwa takribani siku mbili na kuibua hofu kwa wadau wa klabu ya Yanga

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema wamefanikiwa kuwasiliana na Makambo na atawasili nchini wakati wowote

Ufafanuzi

Taarifa ya sintofahamu kuhusu Makambo iliripotiwa jana kwa mara ya kwanza na mtandao wa DaboTen ambao ulidai mshambuliaji huyo alikuwa ametoweka Hoteli alipokuwa akiishi na hakuwa akipatikana kwenye simu

Hata hivyo, Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten alitoa ufafanuzi wa sakati hilo akibainisha kuwa ni kweli Makambo alikuwa ameondoka nchini lakini aliruhusiwa na Kocha Mwinyi Zahera ambaye aliwapa wachezaji wote mapumziko ya siku kadhaa baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City

Makambo alipaswa kurejea nchini juzi lakini uongozi wa timu hiyo ulishindwa kumpata kwenye simu yake ya kiganjani lakini hatimaye leo wameweza kumpata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’