Mashabiki wa Yanga wamshangaza Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2019
Mashabiki wa Yanga wamshangaza Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ametembea nchi nyingi barani Afrika lakini hakuona ushabiki wa soka wa aina yake kama uliopo hapa Tanzania.

Zahera aliyazungumza hayo jana mbele ya waandishi wa habari baada ya kushangazwa na idadi kubwa ya mashabiki wa klabu ya Yanga aliowaona timu hiyo ilipokwenda kucheza mikoani.

Zahera aliwasifu mashabiki wa Yanga na kusema ni kipekee

Zahera amesema hata kwao DR Congo timu kubwa kama TP Mazembe ina mashabiki wengi katika jiji la Lubumbashi tu lakini ikitoka nje ya mji huo haipati uungwaji mkono wa aina hii alioshuhudia hapa Tanzania kwa timu za Yanga na Simba.

"Kule kwetu Congo TP Mazembe ikicheza Lubumbashi mashabiki wake wanajaza uwanja lakini ikitoka nje ya mji haina hata mashabiki 10 wa kuiunga mkono," alisema Zahera.

"Lakini zikicheza FC Barcelona na Real Madrid utasikia mji mzima ukirindima pale moja ya timu hizo inapofunga bao. Lakini hapa Tanzania ni tofauti sana, mashabiki wanapenda sana Yanga na Simba"

Zahera amefichua kuwa moja ya mambo yanayomfanya afurahie kufanya kazi katika klabu ya Yanga licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili klabu hiyo ni upendo wa mashabiki kwa timu yao na ushirikiano anaopata kutoka kwa mashabiki hao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’