Takwimu zaibeba Yanga Mbeya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2018
Takwimu zaibeba Yanga Mbeya

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga kesho watakuwa wanasaka alama tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa katika dimba la Sokoine.

Mchezo huo unakutanisha timu mbili ambazo ziko kwenye ubora tofauti. Yanga iko katika kiwango bora zaidi ikiwa inaongoza ligi na alama zake 47 baada ya kushuka dimbani mara 17. Imeshinda michezo 15 na kutoka sare michezo miwili.

Mbeya City ina alama 23 ikiwa imeshuka dimbani mara 17 pia. Imeshinda michezo sita, imefungwa michezo sita na kutoka sare michezo mitano.

Yanga inaonekana kuwa 'on fire' na kwa hakika kitakachowasaidia Mbeya City kesho labda wenyeji wao kwa kuwa mchezo huo unapigwa kwenye dimba la Sokoine.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amebainisha kuwa wamedhamiria kumaliza kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukamilika kwa mzunguuko wa kwanza, hivyo kupata matokeo katika mchezo wa kesho na utakaobaki dhidi ya Azam Fc ni muhimu

Yanga iko mkoani Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 18 na viongozi wa benchi la ufundi wakiongozwa na kocha Zahera.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’