Hili la mapato ya jezi linahitaji mjadala

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
25 Dec 2018
Hili la mapato ya jezi linahitaji mjadala

Mpaka sasa tunaweza kusema uongozi wa Yanga umeshindwa kubuni mpango mkakati wa kuhakikisha timu inanufaika na mapato ya mauzo ya jezi zenye nembo ya klabu hiyo.

Tangu mwanzoni mwa msimu mashabiki wa timu hiyo wameomba uongozi kuweka hadharani utaratibu au maeneo ambayo wanaweza kununua jezi ili kuiongezea timu mapato.

Jana kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tukuyu Stars Yanga imetambulisha jezi aina nyingine, pengine hilo linaweza kuwa toleo la sita msimu huu. Hali hiyo pia inawachanganya mashabiki kwani wanashindwa kufahamu zipi ni jezi maalum za Yanga msimu huu?

Lakini jambo la msingi hapa ingefaa kuwepo utaratibu (uliotangazwa na uongozi) kuwawezesha mashabiki wanaotaka kununua jezi halisi za klabu kuzipata kwa urahisi.

Usiri huu unawafanya baadhi kuhofia kuwa isije ikawa mpango huo wa jezi unaratibiwa na kuwanufaisha watu wachache ambao pengine ni viongozi wa klabu hiyo.

Pengine viongozi watakaopatikana kwenye uchaguzi wa Januari 13 walifanye hili kuwa ajenda yao namba moja.

Wakati huu mashabiki wanaaswa kuichangia timu ili iweze kusafiri, lakini mashabiki hawa kila siku wamekuwa wakiuomba uongozi uwape utaratibu wa KUNUNUA jezi za timu hiyo bila ya mafanikio.

Hivi kuna njia gani rahisi ya kuiongezea klabu mapato zaidi ya kuuza jezi na bidhaa nyingine ndogondogo za klabu?

Ni vyema uongozi wa Yanga ukajitokeza hadharani kubainisha utaratibu wanaotumia kuuza jezi za klabu hiyo ili kuwaondoa wasiwasi mashabiki na wanachama wake.

Pia waweke hadharani mauzo ambayo yamepatikana tangu kuanza kwa msimu huu. Wanachama wana haki ya kuhoji na kupewa takwimu hizi na isionekane wanaohoji kuwa wanachuki na viongozi waliopo

Timu inahitaji fedha na tayari ina vyanzo vya mapato mkononi ambavyo inaonekana kama havitumiwi ipasavyo ili kuiongezea timu mapato.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’