Wakala afunguka kilichoikwamisha Yanga kumsajili Ilanfya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2018
Wakala afunguka kilichoikwamisha Yanga kumsajili Ilanfya
Wakala wa aliyekuwa mshambuliaji wa Mwadui FC Charles Ilanfya aliyesajiliwa na KMC katika dirisha dogo la usajili baada ya Yanga kushindwa kumalizana nae, amefunguka kilichosababisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ashindwe kusajiliwa na Yanga

Katika mahojiano na Omary Katanga, mtangazaji wa UFM Radio, Shariff Majisafi anayemuwakilisha kinda huyo amesema alimpeleka mteja wake katika klabu ya KMC baada ya Yanga kushindwa kutoa kwa wakati fedha za usajili huku wakishindwa kukubalina kuhusu urefu wa mkataba

Shariff amesema walifika makubaliano na Yanga ya dau la usajili la Mil 15, ambapo Yanga ilipaswa kutanguliza Mil 10 huku Mil 5 zilizobaki zingelipwa kufuatana na makubaliano yao.

Hata hivyo Wakala huyo amesema Yanga ilitaka kulipa Mil 5 kwanza kisha ibaki na deni la Tsh Mil 10.

Pia Shariff amesema Yanga ilitaka kumsainisha kinda huyo mkataba wa miaka mitatu lakini wao walitaka mkataba wa miaka miwili ambao ungekuwa na kipengele cha kumruhusu kwenda kucheza nje ya nchi kama akipata timu

Shariff amesema kutokana na tofauti hiyo , Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika aliomba apewe muda zaidi kuweza kujadiliana na wenzie kabla ya kukamilisha mchakato wa usajili wa Ilanfya

Hata hivyo Shariff amesema aliamua kumpeleka Ilanfya KMC baada ya kuona muda wa kufungwa dirisha la usajili unaelekea ukingoni huku uongozi wa Yanga ukiwa kimya.

Ilanfya amesaini KMC mkataba wa mwaka mmoja.

Ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamependekezwa na kocha Mwinyi Zahera lakini usajili wake ukashindikana mwishoni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’