Yanga mtegoni kusajili kipa mwingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2018
Yanga mtegoni kusajili kipa mwingine
Kwa jinsi hali ilivyo upo uwezekano mkubwa kwa klabu ya Yanga kusajili mlinda lango mwingine kuchukua nafasi ya Beno Kakolanya.

Dirisha dogo la usajili litafungwa siku nne zijazo, Yanga inaweza kulazimika kufanya maamuzi magumu ya kuachana na Kakolanya kama mpaka Ijumaa mwafaka hautafikiwa baina ya pande mbili.

Aidha wasiwasi ulioonyeshwa na kocha Mwinyi Zahera baada ya kubaini wakala wa mlinda lango huyo ni kiongozi wa Simba huenda ukamfanya aondoe imani kwake na anaweza asimuhitaji

Kwa sasa Yanga inamtegemea zaidi kinda Ramadhani Kabwili ambaye amedaka michezo mitano iliyopita na Yanga kushinda yote.

Kabwili amechukua mikoba ya Kakolanya baada ya Mcongomani Klaus Kindoki kushindwa kuonyesha makali yake

Hivyo Yanga bado inahitaji kuwa na mlinda lango mzoefu atayeweza kuhimili mikiki mikiki ya ligi hasa wakati huu ambao ushindani kuelekea ubingwa umeanza kushika kasi

Kumekuwa na taarifa kuwa mabosi wa Yanga hawajakata tamaa ya kumnasa mlinda lango wa Bandari Fc Farouq Shikalo ambaye pia yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’