Kamati ya uchaguzi ya TFF leo inatarajiwa kukamilisha zoezi la usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu ya Yanga
Hata hivyo mchakato huo umekuwa ukisimamiwa na TFF pekee bila ya kuwashirikisha viongozi wa Yanga ambao kimsingi ndio wanaopaswa kumiliki mchakato wote.
Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Samuel Lukumay amesema wamejiweka kando baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa TFF tangu mwanzo
“Nimechaguliwa na klabu kukaimu nafasi ya uenyekiti, nasimamia kanuni za klabu yangu, hatuwezi kushiriki kwenye mchakato ambao hatukushirikishwa hapo awali," amesema
"Wanawafanyia usaili wagombea wao (Kamati ya uchaguzi ya TFF) wanafahamu vipi kama hao wagombea ni wanachama hai wa Yanga?,” alihoji Lukumay.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Ally Mchungahela amesisitiza kuwa wataendelea na zoezi hilo licha ya viongozi wa Yanga kulisusia
“Tuliwapa taarifa kwa barua, tukiwakaribisha kushiriki nasi kwenye zoezi hili, lakini alikuja Mjumbe mmoja tu ambaye naye hakukaa akatoa udhuru na kuondoka"
"Niseme tu sisi tunaendelea na zoezi letu kama tulivyopanga na uchaguzi utafanyika kwa tarehe iliyopangwa,” alisema Mchungahela
Hata hivyo haijafahamika TFF itaitisha vipi Mkutano Mkuu wa Wanachama kwa ajili ya kufanya uchaguzi huo kwani wanaopaswa kufanya hivyo ni viongozi wa Yanga.
TFF haina orodha wala taarifa sahihi za wanachama wa Yanga

ADVERTISE HERE