Nyika na siri ya usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2018
Nyika na siri ya usajili Yanga
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema timu hiyo itakamilisha usajili wa nyota wapya wiki ijayo kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili

Dirisha la usajili lilifunguliwa Novemba 15 na litafungwa Disemba 15, siku kumi zikiwa zimesalia kuanzia leo.

Kumekuwa na majina ya wachezaji yanayotajwa kuwa mbioni kutua Jangwani lakini Nyika amegoma kuweka hadharani majina ya wachezaji walio katika mazungumzo nao hadi pale taratibu zote za usajili zitakapokamilika

Mchezaji pekee ambaye mchakato wake uko wazi ni winga Reuben Bomba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye yuko nchini kukamilisha taratibu za usajili

Wachezaji wengine wanaotajwa ni pamoja na beki wa Lipuli Ally Mtoni 'Sonso' ambaye mwenyewe amekiri kumalizana na uongozi wa Yanga akisubiri kukamilika kwa mazungumzo baina ya Lipuli na Yanga

Mwingine anayedaiwa kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ni winga John Tiber ambaye ameomba aachwe na klabu ya Singida United iliyokimbiwa na wachezaji wengi baada ya kukumbwa na 'ukata'

Wengine ni kiungo Kenny Ally, washambuliaji Nelson Senkatuka (Mganda) , Eliud Ambokile na Vitalis Mayanga

Ikumbukwe pia Yanga itamuongeza kikosini mchezaji wake Mohammed Issa 'Banka' ifikapo Februari 2019 atakapokuwa amemaliza adhabu ya kufungiwa miezi 14.

Banka ataruhusiwa kuanza kujifua na kikosi cha Yanga kuanzia mwezi ujao na ataanza kuitumikia Yanga Februari 08.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
44m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’