Yanga yapania kupamba sherehe za Uhuru

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2018
Yanga yapania kupamba sherehe za Uhuru
Disemba 09, 1961 ndio siku ambayo Tanganyika ilipata Uhuru kisha miaka mitatu baadae April 26 1964 nchi ya Tanzania ikazaliwa baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar.

Jumapili ijayo itakuwa siku ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) sasa ikiwa imepita miaka 57 tangu kujiri kwa tukio hilo la kihistoria.

Siku hiyo pia vinara wa ligi kuu Yanga watashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Biashara United katika mchezo wa ligi hiyo.

Yanga imepania kuifanya siku hiyo kuwa ya furaha kwa mashabiki wake na imewaalika kujitokeza kwa wingi dimba la Taifa kuwashuhudia mabingwa hao wa kihistoria watakapokuwa wakichuana na Biashara United.

"Yanga ni utamaduni wa Mtanzania,ni hazina ya urithi wetu na hifadhi ya mapokeo,ni Tunu ya Wananchi na alama ya Uhuru wetu," imesema taarifa ya Yanga

"Ewe MwanaJangwani usikose Jumapili 9/12/2018 kusherekea siku ya Uhuru kwa kuwatizama mabingwa mara nyingi Tanzania Yanga wakichuana na Biashara toka Musoma alikozaliwa Mpigania Uhuru Baba wa Taifa letu na Shabiki Nguli wa Yanga Hayati Mwl Nyerere.

"Tusherekee Uhuru wetu kwa kuitizama Tunu ya Taifa Letu Yanga...Usikose ewe Mwanachi. Daima mbele nyuma mwiko"

Kwa sasa kikosi cha Yanga kiko Sumbawanga ambapo leo kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Sumbawanga United

Mchezo huo utapigwa saa 10 jioni dimba la Mandela
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’