Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka viongozi wa timu hiyo kuachana na mlinda lango Beno Kakolanya kama hataki kurejea kikosini
Zahera amesema hafahamu mchezaji huyo ana matatizo gani kwani tangu aliporejea kutoka DR Congo alikokwenda kutimiza majukumu ya timu ya taifa, hakuonana nae
Akihojiwa na Azam TV jana kabla ya mchezo wa ligi kuu kati ya Prisons dhidi ya Yanga, Zahera alisema viongozi wa timu hiyo walimtaarifu kuwa Kakolanya aligoma kusafiri na timu.
Hata hivyo mchezaji huyo hakumtaarifu Zahera kuhusu sababu inayomfanya ashindwe kujumuika na wachezaji wengine kambini
"Viongozi waliniambia Kakolanya amegoma kusafiri. Nilitegemea mwenyewe angenieleza sababu inayomfanya ashindwe kutimiza wajibu wake," alsema Zahera
"Hakunipigia simu na hata viongozi wa Yanga hakuwapigia simu. Mimi nimewaambia wamuache. Kwa kuwa hajanieleza matatizo yake mimi siwezi kumpigia simu kumuuliza."
Inadaiwa mlinda lango huyo ana madai kwa klabu ya Yanga yanayomfanya 'ajiweke kando' hadi hapo yatakapomalizwa.

ADVERTISE HERE