Yanga imetua jijini Mbeya tangu jana tayari kwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons maarufu kwa jina la Wajelajela utakaopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Sokoine.
Kikosi hicho ambacho kilikuwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera, mara baada kutua Uwanja wa Kimataifa wa Songwe jana, mashabiki na wanachama wa Yanga jiji Mbeya walijitokeza kwa uwingi kwa ajili ya kuwaunga mkono.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema, mchezo dhidi ya Tanzania Prison si wa kubeza kutokana jinsi kikosi hicho kilivyo jiimarisha katika safu ya ulinzi.
"Tumetua salama Mbeya jukumu lililo mbele yetu ni kusaka ushindi ili tuondoke na pointi tatu. Nina kikosi kizuri na kilicho kamilika kwenye safu ya ushambuliaji.
"Licha ya kuwa sijaongozana na wachezaji wengine kutokana na matatizo tofauti yakiwemo majeraha tunatakiwa kushinda,"alisema Zahera.
"Tunashukuru mashabiki wetu wa Mbeya kwa mapenzi waliyotuonyesha na tunawaahidi kuwa tutawafurahisha siku hiyo ya Jumatatu tutakayokuwa uwanjani"
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE