Mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa uwanja wa Taifa leo, Yanga ndiye mwenyeji.

TFF ilitoa ufafanuzi jana kuwa si kwamba mchezo huo ambao awali ratiba ilikuwa ikionyesha utapigwa mkoani Tanga kuwa umehamishiwa Dar.
Afisa Habari wa TFF Clifford Dimbo amesema mchezo wa leo Yanga ni mwenyeji na mchezo wa mzunguuko wa pili ambao utapigwa February 09 2019, JKT Tanzania itakuwa mwenyeji na utapigwa dimba la Mkwakwani
Mapema wiki hii klabu ya JKT Tanzania iliiandikia barua TFF ikipinga mabadiliko hayo ya ratiba ikitaka mchezo huo wa raundi ya kwanza ukapigwe mkoani Tanga
Ikumbukwe Yanga ndio klabu iliyokuwa na viporo vingi na kama TFF isingefanya mabadiliko hayo Yanga ingecheza michezo minne mfululizo ugenini
Kwani baada ya mchezo wa leo, Disemba 03 Yanga itasafiri mkoani Mbeya kuikabili Tanzania Prisons

ADVERTISE HERE