Uongozi wa klabu ya Yanga huenda ukawaruhusu baadhi ya wachezaji kwenda kuzitumikia timu nyingine kwa mkopo ili kuimarisha viwango vyao.
Klabu ya Namungo Fc kutoka Ruangwa ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza imeonyesha nia ya kumchukua mshambuliaji wa kinda Yohana Mkomola.
Namungo tayari imemnasa kwa mkopo mshambuliaji wa Azam Fc Mbaraka Yusufu na upo uwezekano Mkomola akawa mbioni kutua katika klabu hiyo inayodhaminiwa na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa.
Hata hivyo mpango huo utategemea na uamuzi wa kocha Mwinyi Zahera ambaye amesita kuwaruhusu baadhi ya wachezaji kabla timu yake haijasajili wachezaji aliowapendekeza

ADVERTISE HERE