Yanga imeshindikana mikoani labda ipelekwe Wilayani!

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
26 Nov 2018
Yanga imeshindikana mikoani labda ipelekwe Wilayani!
Baada ya kucheza michezo kumi mfululizo kwenye uwanja wa Taifa na kufanikiwa kushinda nane huku ikitoka sare michezo miwili, wapo walioibeza Yanga.

Wengi hasa mashabiki wa timu pinzani waliamini changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga hazitaiacha salama itakapoanza kwenda kucheza mikoani.

Hata hivyo baada ya ushindi wa michezo yote miwili iliyopigwa kanda ya ziwa dhidi ya Mwadui Fc na Kagera Sugar, wakosoaji hao wamekosa la kusema.

Yanga inayonolewa na kocha Mwinyi Zahera haionekani kuathiriwa kabisa na changamoto zake za nje ya uwanja jambo linalowashangaza wengi.

Mwanzoni wa msimu wengi waliichukulia Yanga kama timu dhaifu na isingeweza kufua dafu msimu huu baada ya kushindwa kufanya usajili mkubwa kutokana na changamoto za kifedha.

Hata hivyo kocha Zahera ameweza kuimarisha viwango vya wachezaji alionao na wamekuwa wakijituma kila wanapopewa nafasi.

Aidha mfumo wa kocha huyo wa kuwapa nafasi wachezaji kulingana na jitihada zao mazoezini bila ya kujali majina yao umeongeza ufanisi kwani kila anayepewa nafasi anajituma zaidi ili kuhakikisha anapata nafasi wakati mwingine

Haishangazi kuona Yanga haina presha ya kusajili wachezaji wapya tofauti na wengi walivyodhani kuwa timu hiyo ingekuwa 'busy' kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Viongozi wa timu hiyo wanaendelea na mchakato wa usajili kwa usiri mkubwa na huenda timu hiyo ikasajiliwa wachezaji wachache kuliko inavyofikiriwa.

Siri kubwa ya uimara wa Yanga ni kocha wao Zahera ambaye kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia na sasa wanaamini wanaweza kushinda kila mchezo unaokuja mbele yao.

Kikosi cha Yanga kiko imara sana kuliko wengi wanavyodhani.

Kikosi hiki cha Zahera kinaweza kumaliza duru ya kwanza na pengine msimu mzima bila ya kupoteza mchezo.

Sababu wachezaji wamekuwa wakijituma sana na katika akili zao hakuna kabisa mawazo ya kufungwa.

Ndio maana mpaka sasa wamecheza miezi mitatu bila ya kupoteza mchezo hata wa kirafiki!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’