Ni dhahiri mlinda lango Klaus Kindoki juzi aliyaweka hatarini maisha yake ya soka ndani ya klabu ya Yanga baada ya 'kuizawadia' Mwadui Fc bao kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania.
Kama sio bao la Mrisho Ngasa lililoihakikishia Yanga alama tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, pengine hali ya mlinda lango huyo aliyebubujikwa na machozi baada ya kutolewa ingekuwa mbaya zaidi.
Kindoki alianza vyema kuitumikia Yanga na kufanya vizuri kwenye michezo kadhaa ya kirafiki wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
Hali iligeuka pale alipoisaidia Stand United kupata mabao matatu katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-3.
Mwanzoni Kocha Mwinyi Zahera alimtetea mlinda lango huyo na aliendelea kumpa nafasi kwenye baadhi ya michezo akisisitiza ni muhimu mchezaji huyo akapewa nafasi ili aongeze kujiamini.
Makosa aliyorudia juzi kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc yalimfanya Zahera ashindwe kumvumilia na akamtoa nje mara moja na kumpa nafasi Ramadhani Kabwili.
Mpaka sasa Kindoki amefungwa mabao manne katika mechi tatu alizodaka, sio uwiano mzuri na amekuwa akirudia makosa yale yale anayofanya michezo ya nyuma.
Huenda mlinda lango huyo akahitaji muda zaidi ili aweze kwendana na kasi la soka la Tanzania.
Lakini ni dhahiri muda huo ataukosa kwani kwa ligi ilipofikia sasa, hakuna nafasi ya majaribio tena

ADVERTISE HERE