Wachezaji Stars matumaini kibaoo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Nov 2018
Wachezaji Stars matumaini kibaoo
Kila Mtanzania mpenda soka leo maombi yake yote itakuwa kwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayoshuka dimbani huko Lesotho dimba la Sesotho kwenye mchezo ambao matokeo ya ushindi yataihakikishia Stars tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.

Hali ni hivyo hivyo kwa wachezaji wa Stars ambao wamesema siku ya leo ni muhimu sana katika maisha yao ya kusakata kabumbu.

Saimon Msuva ambaye leo atakuwa na jukumu kubwa kutokana na kukosekana kwa nahodha Mbwana Samatta anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano, amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo na watahakikisha wanashinda.

"Sisi wachezaji tunatambua umuhimu wa mchezo huo. Tunajua Watanzania wanashauku kubwa ya kuona timu yao inafuzu kwa fainali za AFCON 2019"

"Tunajua wanatuombea basi nasi tutahakikisha hatuwaangushi kwani kila mchezaji pia ana shauku ya kucheza fainali za AFCON"

Mlinda lango Aishi Manula amesema siku ya leo ni ya kipekee kwa soka la Tanzania. Ni siku kubwa ambayo itaingia katika kumbukumbu.

"Tumejiandaa kwa siku 11 nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huu. Tunajua Watanzania wanatuombea ili tuweze kufanya vizuri. Tutahakikisha tunatimiza ndoto ya kila mmoja wetu"

Hassani Kessy anasema mchezo wa leo watahakikisha wanapata matokeo ili waweze kufuzu kwa fainali za AFCON zitakazopigwa mwakani nchini Cameroon.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Tanzania.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’