TFF ilivyokosa msimamo kwa nafasi ya Manji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2018
TFF ilivyokosa msimamo kwa nafasi ya Manji Yanga
Baada ya kikao cha kamati ya Utendaji Yanga na Kamati ya uchaguzi ya TFF kufikia Maamuzi ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi ikiwemo ya Mwenyekiti, TFF imedhihirisha jinsi inavyofanya maamuzi kwa kukurupuka

Maamuzi ya kikao hicho kilichofanyika leo Ijumaa, Novemba 16 ni baada ya kuafikiwa kuwa Katiba ya Yanga haiwapi Wanachama mamlaka ya kumrejesha madarakani kiongozi aliyejiuzulu.

Lakini Julai 11 2018 Shirikisho la soka nchini (TFF) lilimuondoa kwenye nafasi yake aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Clement Sanga baada ya kupokea barua kutoka kwa uongozi wa Yanga ikimtambulisha Yusufu Manji kuwa amerejea klabuni hapo.

Sanga aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga alipoteza sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi baada ya TFF kuikubali barua ya Yanga iliyomtambulisha Manji kuwa Mwenyekiti baada ya kuridhia kurejea.

Sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu ni lazima uwe Mwenyekiti wa timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Hata hivyo uamuzi huo uliotolewa miezi minne iliyopita na TFF ni kinyume kabisa na uamuzi wao wa sasa wa 'kuilazimisha' Yanga ichague Mwenyekiti mwingine licha ya kuwa walishamtambua Manji na uamuzi wao huo ulisababisha Sanga akapoteza kibarua chake kwenye Bodi ya Ligi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’