Usiku wa kuamkia leo, Esperance ya Tunisia imefanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Afrika msimu wa 2017/18 baada ya kuifumua Al Ahly mabao 3-0.
Esperance imeshinda taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 kwani katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Misri walifungwa 3-1
Hilo ni taji la tatu kwa Esperance ambayo sasa imekata tiketi kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo katika msimu huu unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Licha ya kutwaa kombe, Esperance itapokea kitita cha fedha zaidi ya Bil 2.5 kutoka CAF huku Al Ahly ikikunja zaidi ya Bil 1.5
Simba itashiriki michuano hiyo msimu huu baada ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita.
Imepangiwa kuanzia nyumbani dhidi ya Mbabane Swallows, timu aliyotoka kiungo wa Yanga Papi Tshishimbi.
Swallows ilitinga hatua ya makundi msimu uliomalizika ikipangwa kundi D na Etoile Du Sahel, 1st De Agosto na ZESCO.
Simba inapaswa kujipanga kwelikweli kuweza kuwaondosha Waswazi hao ambao miaka ya hivi karibuni ni kawaida kwao kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE