Tshishimbi, Kamusoko waipendezesha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2017
Tshishimbi, Kamusoko waipendezesha Yanga
Viungo Thabani Kamusoko na Papi Tshishimbi watatengeneza umoja wa hatari, dalili zimeanza kuonekana mapemaaa.

Kwa mara ya kwanza jana viungo hao wawili walicheza pamoja kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri, wakiingia kwenye kipindi cha pili.

Uwepo wa Tshishimbi unampa Kamusoko uhuru wa kusogea mbele na kuwatengenezea nafasi washambuliaji.

Licha ya kuwa alicheza kwa dakika 45 pekee, Tshishimbi alihusika kwenye matukio 48 ya mchezo huo. Alipiga pasi 40, kapokonya mipira mara 3, kajaribu mashuti ya langoni mara 2 na alifanyiwa madhambi mara 3.

Kiungo huyu anaijua vyema kazi yake, yuko kila mahali dimbani. Timu ikiwa inashambuliwa yuko langoni kuzuia na pia timu ikiwa inashambulia yuko langoni kwa adui kuongeza nguvu.

Ana pumzi, ana nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi sahihi pale anapokuwa na mpira mguuni kwake.

Pia ikumbukwe ndio kwanza amefanya mazoezi kwenye kikosi cha Yanga kwa siku mbili tu.

Kwa muda mchache aliocheza jana, akishirikiana vyema na Kamusoko na Alpha waliweza kubadili aina ya uchezaji wa Yanga. Unaweza kusema kwa muda huo tuliweza kuiona ile Yanga ya Pluijm ambayo wengi walikuwa wakiamini ametoweka nayo.

Ile Yanga iliyokuwa inaweza kupiga mpaka pasi 30 bila kupoteza mpira tuliishuhudia jana. Jana Yanga ingeweza kushinda kwa mabao hata matatu kama washambuliaji Ajib na Ngoma wangezitumia vyema nafasi kadhaa walizopata.

Ni dhahiri keshokutwa Jumatano Simba itakuwa na wakati mgumu sana kwenye dimba la Taifa. Tshishimbi ameimarisha safu ya kiungo ya Yanga mara dufu kama ilivyotarajiwa.

Kuwa na viungo wazuri wanaojuwa vyema majukumu yao kunapunguza kwa kiasi kikubwa presha kwa walinzi. Safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa inaonekana kuwa na mapungufu kwa kuwa kulikuwa na madhaifu sehemu ya kiungo mkabaji.

Lakini uwepo wa Tshishimbi utapunguza presha hiyo kwani moja ya kazi anazozimudu dimbani ni kulinda safu yake ya ulinzi.

Kwa namna kocha George Lwandamina alivyokipanga kikosi chake katika kipindi cha pili, ni wazi kwenye mchezo dhidi ya Simba atatumia viungo watatu, akimpanga Tshishimbi kama namba sita, Kamusoko namba nane na Raphael Daudi, akicheza nyuma ya straika kama namba 10.

Katika safu ya ushambuliaji huenda akaanza na Ajib, Ngoma na Emanuel Martin mfumo ukitarajiwa kuwa 4-3-3
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’