Yondani ataukosa mchezo dhidi ya Ndanda Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2018
Yondani ataukosa mchezo dhidi ya Ndanda Fc
Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani ataukosa mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Ndanda kutokana na majeraha ya goti aliyopata mchezo uliopita.

Hata hivyo Andrew Vicent Chikupe amerejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kukosekana kwa wachezaji hao hakumpi hofu kwani wapo wengine watakaocheza na kuziba nafasi zao.

Kikosi cha Zahera pia kitamkosa Geofrey Paulo 'Boxer' anayetumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo dhidi ya Lipuli

Zahera amesema timu yake imejiandaa kikamilifu na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo wa keshokutwa.

"Kukosekana kwa Yondani na Boxer kumenifanya nibadili mfumo wa uchezaji katika mchezo wangu na Ndanda niliokuwa nautumia katika michezo iliyopita kila mtu anafahamu kasi ya mabeki hao katia kupeleka mashambulizi.

"Timu yangu imejiandaa vema kuhakikisha inaendeleza rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo wa ligi katika uwanja wetu wa nyumbani kabla ya kutoka katika mcheo ujao wa ligi.

"Kabla ya ligi kuanza tukiwa kambini Morogoro niliwaambia wachezaji wangu hatutakiwi kupoteza mchezo katika uwanja wetu ni lazima tushinde ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa," amesema Zahera
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
43m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’