Wachezaji wanne kutua Yanga dirisha dogo la usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2018
Wachezaji wanne kutua Yanga dirisha dogo la usajili
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefunguka kuwa timu hiyo imefanya mazungumzo na wachezaji wanne ambao wanaweza kutua Jangwani wakati wa dirisha dogo la usajili linalofunguliwa wiki mbili zijazo.

Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa habari leo, Zahera amesema uongozi wa Yanga uko mbioni kumalizana nao tayari kutua jangwani.

Hata hivyo Zahera hakutaja majina ya wachezaji hao wala timu wanazotoka.

"Kuna wachezaji wanne tumeshazungumza nao tunangoja tu mambo yakamilike kufuatana majadiliano kati yao na uongozi wa Yanga," amesema

"Yuko mshambuliaji mmoja anatoka Ghana, yuko kiungo mmoja anacheza Gabon yeye ni Mcongoman na mkataba wake unamalizika mwezi huu."

"Pia yuko winga mmoja kutoka Congo pamoja na mlinzi wa kati"

Yanga bado ina nafasi tano za wachezaji wa kigeni ili kukamilisha idadi ya wachezaji 10 walioruhusiwa na TFF.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’