Vijana wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho - Nadir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2018
Vijana wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho - Nadir
Meneja wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema leo asubuhi timu imefanya mazoezi kwenye uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc.

Nadir aliyerejea hivi karibuni kutoka Kusini mwa Tanzania alikokwenda kuzindua Matawi ya Yanga wilaya za Masasi na Ruangwa, amesema wachezaji wote waliokambini wako tayari kwa mchezo huo.

Aidha Nadir amedokeza kuwa hali za majeruhi Ibrahim Ajib na Papi Tshishimbi zinaendelea vizuri na kama madaktari wa timu hiyo watatoa ruhusa ya kuwatumia hapo kesho, basi watakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Lipuli Fc.

"Ajib na Tshishimbi wanaendelea vizuri lakini bado wako chini ya uangalizi wa daktari. Hatma yao kuhusu kucheza mchezo wa kesho ama la itatolewa na daktari wa timu," amesema Nadir
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’