Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amesema aliyekuwa mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu aliyehamia Yanga, atawasumbua katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu.
Kichuya amenukuliwa na mtandao wa SalehJembe akisema kuwa uwepo wa Ajibu Yanga, utawasumbua katika mchezo wa Jumatano kwa kuwa wanaujua vilivyo uwezo wake.
"Ajibu ni mchezaji mzuri, hakuna asiyemjua na ni mchezaji mwenye ushindani kutokana na kiwango chake.
"Atatuletea changamoto kubwa katika mchezo huo kwani ni miongoni mwa wachezaji wenye viwango, lakini kwa upande wetu tumejipanga vizuri kuelekea mchezo huo ambao una msisimko mkubwa," alisema Kichuya.
Simba na Yanga zote zipo Zanzibar kujiandaa na mchezo huo wa Ngao ya Jamii unaokaribisha msimu mpya wa 2017/18.

ADVERTISE HERE