Ngasa awashukuru mashabiki wake wa kumuunga mkono

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Oct 2018
Ngasa awashukuru mashabiki wake wa kumuunga mkono
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagam, winga wa Yanga Mrisho Ngasa amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumuunga mkono licha ya changamoto nyingi zailizomkabili.

Ngasa amesema kuna wakati alikata tamaa kutokana na changamoto zilizomkabili lakini ushirikiano alioupata kutoka kwa wadau mbalimbali umemfanya leo awe hapo alipo.

"Mpaka sasa sijui cha kuwalipa Watanzania kwa upendo wao kwanguKuna Kipindi nilihisi mimi sio kitu tena kwenye maisha nilipotea na hakuna thamani yoyote niliyopata kwa kila binadamu na marafiki walinikimbia nikabaki mimi

"Lakini watu hawakujua nilipitiwa na matatizo gani, nikatoka South, Oman, Mbeya City na kisha Ndanda na mwalimu Mlale aliniambia nakupenda na nitakupa nafasi ya kucheza, sikuamini na niliona kama muujiza, na ndoto yangu bado ilikuwa kurudi kucheza timu kubwa.

"Kuna siku nilikutana na Haji Manara (msemaji wa Simba) nikiwa Mbeya City akaniambia "Ngassa wewe ni Tanzania na ukinza kufunga utasikika tu" nilimwambia Ahsante.

"Nilienda Ndanda nikiwa na kiu ya kufanya vizuri lakini hata wakati nasajili Yanga nilikumbuka ushauri wa anko Haji Manara kwamba nijitume.

"Mechi dhidi ya Simba niliandaa dozi lakini sikupata nafasi lakini niliona ni sawa

"Ni kama kinachomtokea Ibrahim Ajib kwani mwalimu ana ndoto nyingi kuhusu Ibra, na anachofanya kocha anampa machungu ili afike mbali zaidi

"Niishie hapa lakini Watanzania tusimseme mtu kwani hatujui anayopitia, mimi anko nacheka na kila mtu, maadui na marafiki, Love U Tanzania n Enjoy Soccer"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’