Taifa Stars kuweka kambi Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2018
Taifa Stars kuweka kambi Afrika Kusini
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajiwa kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za AFCON 2019 dhidi ya Lesotho.

Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe imesema maandalizi ya Kambi hiyo yanaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Oktoba 25, 2018, Dk Mwakyembe amesema michango ya Watanzania na Taasisi mbalimbali bado inahitajika kwa safari ya Taifa Stars kuweka kuweka kambi nchini Afrika Kusini.

β€œTunafuatilia kwa makini Kambi hiyo ya Afrika Kusini hatujaingia kichwa kichwa, tupo makini sana. Wizara yangu, TFF na Wizara ya Mambo ya Nje tunashirikiana kwa ukaribu kuhakikisha kambi nzuri ya Afrika Kusini na salama kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho.

"Tunawashukuru wote waliochangia katika safari ya Cape Verde, bado tunawaomba mchango wao wa hali na mali kuelekea mchezo wa Lesotho TFF na Wizara tunashirikiana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri ya mchezo huo.

"Gharama za kuisafirisha Taifa Stars zimeongezeka zaidi ya bajeti ya awali kutokana na kambi ya nje ya nchi (Afrika Kusini), tunazungumza na mashirika ya ndege tupate bei nzuri, pia kampuni za mabasi ili Watanzania wengi waende kuishangilia timu yao,” amesema Waziri Mwakyembe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’