Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajiwa kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za AFCON 2019 dhidi ya Lesotho.
Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe imesema maandalizi ya Kambi hiyo yanaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Oktoba 25, 2018, Dk Mwakyembe amesema michango ya Watanzania na Taasisi mbalimbali bado inahitajika kwa safari ya Taifa Stars kuweka kuweka kambi nchini Afrika Kusini.
βTunafuatilia kwa makini Kambi hiyo ya Afrika Kusini hatujaingia kichwa kichwa, tupo makini sana. Wizara yangu, TFF na Wizara ya Mambo ya Nje tunashirikiana kwa ukaribu kuhakikisha kambi nzuri ya Afrika Kusini na salama kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho.
"Tunawashukuru wote waliochangia katika safari ya Cape Verde, bado tunawaomba mchango wao wa hali na mali kuelekea mchezo wa Lesotho TFF na Wizara tunashirikiana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri ya mchezo huo.
"Gharama za kuisafirisha Taifa Stars zimeongezeka zaidi ya bajeti ya awali kutokana na kambi ya nje ya nchi (Afrika Kusini), tunazungumza na mashirika ya ndege tupate bei nzuri, pia kampuni za mabasi ili Watanzania wengi waende kuishangilia timu yao,β amesema Waziri Mwakyembe.

ADVERTISE HERE