Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema amewaandaa vijana wake kikamilifu tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa kesho Alhamisi uwanja wa Taifa
Mcongoman huyo aliyefanikiwa kubadili Yanga ndani ya muda mfupi, amepania kuiduwaza KMC iliyopanda daraja msimu uliopita.
"Tumejiandaa vyema kama ambavyo huwa tunajiandaa michezo mingine kikubwa ni kwamba tutaingia uwanjani na kucheza kwa aina ya tofauti kidogo," amesema Zahera
"Tunatambua timu ambayo tunacheza nayo inashiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu lakini siwezi kuwabeza maana wana mwalimu na wachezaji wazuri pia"
Kesho Yanga itashuka dimbani kwa mara ya nane ikiwa imejikusanyia alama 19 kutoka michezo saba iliyocheza mpaka sasa huku pia ikiwa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi
KMC inashika nafasi ya 14 ikiwa imejikusanyia alama 10 kutoka michezo 10 iliyocheza.

ADVERTISE HERE