Kamusoko 'yuleee' ameanza kurejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2018
Kamusoko 'yuleee' ameanza kurejea
Thabani Kamusoko anafahamika kwa uwezo wake wa kutawala dimba na kupiga pasi zenye akili mpaka kupeleka kuibuka kwa jina la 'kampa-kampatena'

Katika michezo ya hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekuwa akimtumia kama 'super-sub' na mara nyingi anapoingia anabadili sura ya mchezo.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance, ni Kamusoko aliyeanzisha shambulizi lililopeleka kufungwa kwa bao la tatu liliwekwa kambani na Ibrahim Ajib.

Kamusoko alimpenyezea pasi Kaseke aliyewazidi mbio walinzi wa Alliance kisha kumtengea mpira Ajib.

Pia alitoa pasi kama hiyo kwa Ngasa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi na kupelekea bao lililofungwa na Emmanuel Martin

Kuimarika kwa kiwango cha Kamusoko ni habari njema sana kwa Yanga ambayo imedhamiria kurejesha ubingwa iliyoupoteza kwa Simba msimu uliopita.

Kesho Alhamisi Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili KMC katika mchezo utakaopigwa saa moja usiku.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’