Kakolanya apania kuweka rekodi ya kutofungwa mabao mengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2018
Kakolanya apania kuweka rekodi ya kutofungwa mabao mengi
Kipa Beno Kakolanya wa Yanga anataka kutengeneza rekodi yake ya kipekee kwa kutoruhusu magoli mengi akiwa na kikosi hicho msimu huu.

Kakolanya akiwa ameidakia timu hiyo michezo mitano ya Ligi Kuu mpaka hivi sasa, ameruhusu bao moja tu kutingisha nyavu zake dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Kakolanya amesema mwenendo huo unamfanya azidi kujituma zaidi uwanjani ili kuhakikisha anaendeleza rekodi yake na kujiweka kwenye mazingira ya kukuza kipaji chake.

β€œHili ni jambo ambalo kipa yoyote anapenda kuwa nalo, najisikia furaha lakini pia sio kwangu tu bali timu nzima kwa sababu inafanya vizuri,” alisema.

Aliongeza zaidi kwamba siri ya yeye kufanya vizuri ni kuwapanga vizuri na mabeki wake uwanjani na kuhakikisha kwamba, hata ikitokea kosa kwa mmoja basi mwingine analiziba.

β€œHuwa nazungumza sana ninapokuwa uwanjani kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi yake vizuri, nashukuru wapo makini na tunakwenda sawa,” alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’