Zahera akoshwa na kipaji cha Ajib, amtaka aongeze juhudi zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Oct 2018
Zahera akoshwa na kipaji cha Ajib, amtaka aongeze juhudi zaidi
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib ni mchezaji anayetumia akili nyingi anapokuwa dimbani.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Alliance, Zahera amesema Ajib ana uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi anapokuwa na mpira na hadhani kama kuna mchezaji anayeweza kumfikia hapa Tanzania.

"Kwa wachezaji wote wanacheza ligi kuu Tanzania hapa hakuna ata mmoja anaweza kuwa na akili ya mpira kama aliokuwa nayo Ajibu," amesema Zahera

"Yeye kabla hujampatia mpira tayari ameshajua nini aufanyie, kinachotakiwa sasa na aongeze nguvu sana na kupambana vyakutosha ili awe bora zaidi."

Ajib amehusika katika mabao yote matatu ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Alliance, akifunga moja na kutengeneza mawili.

Hata hivyo Zahera amemtaka Ajib kuwa na mwendelezo wa kiwango wa chake.

"Ajib anahitaji kubadilika. Awe na mwendelezo wa kiwango chake. Sio leo anafanya vizuri kesho anashuka chini. Inatakiwa awe anapanda kila mchezo"

Alipoulizwa kuhusu maoni yake kama anaona ni wakati sahihi kwa Ajib kuitwa timu ya Taifa, Zahera amesema hana shaka kuwa Ajib anaweza kuchezea timu ya Taifa.

Lakini amemtaka aongeze juhudi na kujituma zaidi anapokuwa dimbani kwani kucheza timu ya Taifa si 'lelemama'
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’