Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe, amesema kwamba ndege ya serikali 'Dream Liner' haitosafirisha kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania, baada ya kupata changamoto ya uwanja wa kutua huko Cape Verde.
Awali, ndege hiyo ndio ilikuwa ikipigwa chapuo lakini imebidi wabadilishe kutokana na changamoto ya uwanja wa kutua.
"Tumemtuma Mgohi aweze kuangalia namna sehemu ilivyo tutakayofikia, ametuambia kwamba uwanja ni mdogo kwahiyo tumeongea na wenzetu wa Airt Tanzania na tumeagiza ndege nyingine ambayo ina usajili wa Tanzania ambayo ina weza kushuka na kupaa kiurahisi," alisema.
Stars inatarajiwa kuondoka leo Jumanne saa tano usiku kwenda Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.
Katika hatua nyingine walinda lango Beno Kakolanya na Abdulrahman Mohammed huenda wakakosa safari hiyo baada ya kupata majeruhi.
Kakolanya alipata majeraha ya nyama za paja kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Mbao FC juzi wakati Abdulrahman anasumbuliwa na jeraha la enka.
Walinda lango Benedictor Tonoko wa Mtibwa Sugar na Aaron Kalambo wa Prisons huenda wakaongezwa kwenye kikosi cha Stars kuchukua nafasi zao.

ADVERTISE HERE