Bossou atishia kuishitaki Yanga FIFA

Admin By Admin
β€’
18 Aug 2017
Bossou atishia kuishitaki Yanga FIFA
Mlinzi wa zamani wa Yanga Vicent Bossou amesema anakusudia kupeleka malalamiko kwenye shirikisho la soka duniani (FIFA) kama hatalipwa madai yake ya mishahara ya miezi miwili.

Kwa mujibu wa mtandao wa BIN ZUBEIRY, Bossou kupitia kwa wakala wake Mganda Gibby Kalule, amesema kwamba viongozi wa Yanga, Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa na Mhasibu, Baraka Deusdedit wamekuwa wakipuuza jitihada zake za kudai malimbikizo yake hayo hata baada ya kuondoka.

Bossou amesema ametuma barua pepe kwa Katibu Mkuu, Mkwasa pamoja na Mhasibu wa Yanga Deusdedit, anasubiri majibu kwa viongozi hao kabla hajachukua hatua zaidi.

Ò€œNasubiri wanijibu barua yangu na kunilipa fedha zangu iwapo wakishindwa kufanya hivyo meneja wangu atachukua hatua zaidi,Ò€ alisema Bossou.



Uongozi ni vyema ukamalizana na mchezaji huyo kama madai yake ni ya kweli. Bossou ameitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa, haina haja ya kupelekana FIFA.

Kwa hakika kuna ulazima wa Yanga kubuni vyanzo vipya vya mapato haraka iwezekanavyo ili kujinusuru na haya yanayotokea sasa.

Kipindi hiki ni kigumu sana kwa viongozi wa Yanga wakiongozwa na Katibu Mkuu, natumai wataivusha timu salama.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’