Jana kipa Beno Kakolanya aliwapa simanzi mashabiki wa Yanga baada ya kupata majeraha na kushindwa kumaliza dakika 90 za mchezo dhidi ya Mbao FC.
akolanya aliumia kwenye kipindi cha kwanza na baadae kujitonesha kwenye dakika 54 baada ya kuruka angani kutaka kuokoa krosi ya Beki wa Mbao, Amos Charles.
Baada ya kukaa chini mashabiki wa Simba waliofika uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo walinyanyuka vitini na kuanza kushangilia kuumia kwa kipa huyo.
Mashabiki hao bado 'wanaweweseka' kutokana na uwezo aliouonyesha Kakolanya kwenye mchezo wa watani wa jadi kwa kuokoa michomo mingi katika pambano lililomalizika kwa 0-0.
Waliamini kutoka kwa Kakolanya kungewapa nafasi Mbao FC kuweza kusawazisha bao hasa baada ya kuingia kwa Mcongoman Klaus Kindoki
Hata hivyo Kindoki hakuruhusu bao huku akiokoa moja ya michomo hatari iliyokuwa inaelekea wavuni.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo huo.

ADVERTISE HERE