Amunike aahidi kuipeleka Stars AFCON 2019

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Oct 2018
Amunike aahidi kuipeleka Stars AFCON 2019
Nyota wa zamani wa Nigeria Emmanuel Amunike anayekionoa kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars amesema amesikia kilio cha Watanzania wanaotaka kuiona timu yao ikifika mbali katika michuano wanayoshiriki na atapambana kwa kutumia nyota wake kufanikisha hilo.

Amunike alisema anajua Watanzania wamekuwa wakiziangalia timu nyingine zikishiriki mashindano mbalimbali, lakini kwa sasa ni muda wa Stars kufanya mambo kama miaka ya nyuma.

β€œMechi dhidi ya Cape Verde itakuwa sio rahisi kwetu hilo linajulikana, ila nimekuwa nikiongea mara kwa mara na wachezaji tuungane na tujitume kuipigania nchi.

"Hakuna jambo zuri kama kuona nyuso ya furaha usoni kwa mtu wako wa karibu na hilo ndio Watanzania wanakihitaji hivi sasa,” Amunike amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Amunike alifunguka zaidi kwa kusema atatumia mbinu tofauti na alizotumia katika mchezo dhidi ya Uganda ili kuhakikisha anapata matokeo dhidi ya Cape Verde.

Cape Verde itacheza na Stars, Oktoba 12 nchini humo kabla ya kurudiana Oktoba 16 wakiwani tiketi ya Fainali ya Afrika (Afcon 2019) zitakazofanyika Cameroon mwakani.

Matokeo ya ushindi au sare kwenye mchezo wa kwanza ugenini yataiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufuzu kama itashinda michezo yake miwili ya nyumbani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’