Ten awaalika mashabiki uwanja wa Taifa Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Oct 2018
Ten awaalika mashabiki uwanja wa Taifa Jumapili
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa keshokutwa Jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa moja usiku.

Ten amewataka mashabiki 'kutokelezea' dimbani wakiwa wamevalia uzi wa Yanga ili kuupendezesha uwanja na kuongeza hamasa kwa wachezaji.

"Njoo umevaa jezi yako ya njano uje uone soka safi lisilo na ngumi kutoka kwa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Tanzania, " amesema Ten.

Ten ameweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo ni Tsh 15,000/- kwa VIP A; Tsh 10,000/- kwa VIP B na C; na Tsh 5000/- upande wa mzunguuko.

Yanga iliyoanza vyema msimu, imepania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo dhidi ya Simba Jumapili iliyopita.

Iko nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 13 baada ya kushuka dimbani mara tano.

Ndio timu iliyocheza michezo michache zaidi kwenye ligi ambayo imeingia raundi ya tisa leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’