Yanga yapania alama tatu mchezo dhidi ya Mbao FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Oct 2018
Yanga yapania alama tatu mchezo dhidi ya Mbao FC
Keshokutwa Jumapili October 07 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa tisa.

Kuelekea mchezo huo, kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwahakikishia wamejipanga kuondoka na alama zote tatu.

Mwandila ataiongoza Yanga kwenye mchezo huo kutokana na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera kuwa na majukumu na timu ya taifa ya Kongo.

"Tunaendelea na maandalizi, mashabiki wasiwe na shaka…tumetoka kupata sare mchezo uliopita, lakini hiyo haina maana hatuwezi kupata ushindi Jumapili,” amesema Mwandila.

Amesema yapo maelekezo aliyoachiwa na Zahera na atayafanyia kazi kuhakikisha Yanga inapata ushindi kwenye mchezo huo wa Jumapili.

“Wachezaji wanaendelea mazoezi na kila mmoja yupo vizuri… yapo mambo kidogo tunayafanyia kazi ya kiufundi ili tuweze kufanya vizuri,” alisema.

Yanga wanaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →