Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amempa majukumu Msaidizi wake, Noel Mwandila kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC wakati yeye akienda kutekeleza majukumu ya timu ya taifa ya nchini kwao DR Congo.
Zahera amesema amemwachia msaidizi wake huyo program zote za mazoezi.
"Siwezi kukwambia programu gani nimemuachia, ila kwa vile naenda nyumbani nimempa kazi Mwandila ahakikishe tunazoa alama tatu mbele ya Mbao FC," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti.
"Namuamini na naamini atayafanyia kazi kikubwa ninachotamani zaidi nisikute kimebadilika ni kupoteza pointi tatu hasa katika michezo ya nyumbani.
"Ni mipango ambayo tuliipanga kabla ya ligi kuanza baada ya kutazama ratiba tulikubaliana kuhakikisha tunavuna pointi zote nyumbani," alisema.
Zahera alisema majukumu aliyonayo katika taifa lake ni muhimu sana na ndio maana kaamua kuondoka mapema kuhakikisha anaisimamia timu yake hiyo ya Taifa kupata matokeo mazuri na kupata nafasi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Afcon.
Yanga imeshinda michezo minne kati ya mitano iliyocheza, ikiambulia sare dhidi ya Simba, huku ikizifunga Mtibwa Sugar (2-1), Coastal Union (1-0), Stand United (4-3) na Singida United 2-0 na kufikisha alama 13 ikiwa nafasi ya nne.

ADVERTISE HERE