Zahera amepania kumaliza duru ya kwanza bila kupoteza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2018
Zahera amepania kumaliza duru ya kwanza bila kupoteza
Yanga mambo ni moto hii ni baada ya kutoka suluhu na watani wao wa jadi Simba, sasa kocha Mkongo Mwinyi Zahera anakuja na mpango mkakati wa namna atakavyohakikisha anamaliza ngwe ya kwanza bila kufungwa.

Zahera amekiri kuwa mechi yao dhidi ya Simba, ilikuwa inamuumiza akili namna ambavyo mashabiki waliichukulia kwa uzito kiasi kwamba ilikuwa inampa picha ya kuona wametembea na matokeo mfukoni.

"Hii si kwa Yanga pekee, hata mashabiki wa Simba kwa namna walivyokuwa na shamla shamla na mechi hiyo inaona wazi kwamba wameishashinda kabla ya dakika 90.

"Jambo ambalo ni changamoto kwa kocha wa aina yoyote Duniani kufanya ovyo mbele ya umati wa maelfu waliofika kuunga mkono timu yao, lakini pia endapo ukishinda mechi unaibuka shujaa, hilo lilinifanya nitumie mbinu za hali ya juu kuhakikisha hatupotezi mbele ya Simba."

Zahera anasema ligi itakapoanza baada ya timu ya taifa kumaliza majukumu yake, anaamini atakuwa na mbinu mpya ambazo zitamfanya mzunguko wa kwanza wajikite kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo .

"Nimejiwekea mikakati ya mzunguko wa kwanza nisipoteze. Nikifanikiwa nitaingia mzunguko wa pili kuelekea ubingwa, lengo ni kuona namna ambavyo tutafanya timu isipoteze mchezo hata mmoja ingawa tunajua kuna ushindani wa hali ya juu,"anasema Zahera.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’