Majeruhi yatesa makipa Yanga

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
17 Aug 2017
Majeruhi yatesa makipa Yanga
Kipa mpya wa Yanga Youthe Rostand 'mikono buku' anatarajiwa kuwa fit kuivaa Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Jumatano ijayo, August 23.

Awali Rostand alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo huku Beno Kakolanya akiondolewa kambini kutokana na majeraha.

Wachezaji wengine ambao wameondolewa kambini na hawataweza kuivaa Simba kutokana na kuwa majeruhi ni Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya.

Rostand ameshaanza mazoezi huku kocha wa makipa Juma Pondamali akiwatoa hofu mashabiki wa Yanga kuwa anategemea atakuwa fit kuwa langoni kwenye mchezo dhidi ya Simba Jumatano ijayo.

Kipa chipukizi Ramadhani Kabwili alipewa majukumu ya kusimama baina ya milingoti mitatu katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting na Mlandege baada ya Beno na Rostand kuwa majeruhi

Kabwili pia anaweza kuwa langoni kwenye mchezo wa ngao ya Jamii kama Rostand hatakuwa sawa.

Aidha Meneja wa Yanga, Hafidh amesema kambi imezidi kunoga na kueleza sababu ya kwenda kujificha Pemba, akisema kuwa inatokana na hali ya utulivu uliopo visiwani humo na kutoa nafasi kwa wachezaji kupata nafasi nzuri ya kujifunza vema mbinu za makocha wao.

Alisema siku zote kambi yao ya Pemba huwa haijawaacha Simba salama, kitu anachoamini hata sasa wanaweza kufanya kweli wakitokea huko.

Ò€œHali ya utulivu ni sababu ya kukimbilia huku, wachezaji wapate nafasi ya kushiba mbinu za makocha kabla ya kuvaana na Simba, tunaamini tutaendeleza moto wetu mbele ya watani,Ò€ alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’