Baada ya kukosa ushindi wanasingizia uchawi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2018
Baada ya kukosa ushindi wanasingizia uchawi
Ni kawaida kwa mashabiki wa Simba kuingia uwanjani na matokeo mfukoni kwenye michezo dhidi ya Yanga.

Hili huwa linasababishwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuwaaminisha mashabiki wao kuwa wana timu bora ambayo inaweza kuibuka na ushindi kila inaposhuka dimbani.

Sasa mambo yanapokwenda tofauti, viongozi hao wanalazimika kutafuta mbinu ya kutuliza 'kelele' za mashabiki.

Ndio maana wakati mwingine wanadiriki kwenda na TV mbele ya waandishi wa habari ili kuwaaminisha mashabiki kuwa wanaonewa!

Baada ya kulazimishwa sare na Yanga jana, mjadala mkubwa ulio kwenye mitandao ya kijamii ni tuhuma za ushirikina. Eti Yanga haikufungwa sababu iliroga!

Wamesahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu, yaani kushinda, kushindwa na kutoka sare.

Badala ya kuwalaumu washambuliaji wao waliopoteza nafasi nyingi za kufunga, viongozi wa timu hiyo wanawaaminisha mashabiki kuwa ni sababu ya uchawi wa Yanga!

Kama uchawi ungekuwa unacheza mpira basi nadhani Nigeria wangekuwa vinara wa kutwaa taji la kombe la dunia!

Lakini mwezi Juni mwaka huu tumeshuhudia kule Urusi wakipewa vipigo vya 'mbwa koko' na kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la dunia mapema tu.

Hata hapa Tanzania kuna mikoa inasifika kwa kuwa na imani za kishirikina mfano Rukwa lakini hawana timu inayoshiriki ligi kuu!

Lakini jambo jingine la msingi wanasahau kuwa hakuna timu ambayo itakwenda uwanjani ikiwa na lengo la kufungwa, labda iwe imehongwa.

Eti wanashangaa Ajib kuanzisha mpira kwa kupiga nje. Kana kwamba hilo ni jambo la ajaaabu!

Kwa wanaofuatilia kweli soka duniani wanafahamu Ajib hakuwa mchezaji wa kwanza kuanzisha mpira kwa kuutoa nje.

Alichokifanya Ajib ni kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na kocha wake.

Kilichofanywa jana na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ni kubadili mbinu tu za mchezo na kuwakabidhi mpira Simba wamiliki kwa muda mwingi huku Yanga ikitumia mashambulizi ya kushitukiza.

Ajib alitoa mpira nje ili kujipanga na ukelezaji wa mfumo huo waliopanga kuutumia kwenye mchezo.

Yanga haikuwa na cha kupoteza jana. Zahera hakutaka timu yake ifungwe alilifanikisha hilo, anastahili pongezi yeye na wachezaji wake kwani walifanikiwa kimbinu.

Mashabiki wa Yanga wana haki ya kushangilia matokeo ya jana kwa kuwa yameinufaisha timu yao. Yanga imeendeleza rekodi ya kuanza msimu vizuri kwa kutofungwa.

Lakini pia imefikisha alama 13 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo! Pia bado ina mchezo mmoja wa kiporo ambao kama ikishinda itaongoza ligi.

Hali ni tofauti kwa Simba, sare imewafanya wabaki nafasi ya tano. Tambo za ubora wa kikosi chao hazilingani na matokeo wanayoyapata uwanjani.

Mpaka sasa wamepoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili. Hizi ndizo takwimu walipaswa wazijadili na sio kusingizia mambo ya uchawi.

Yani timu imecheza michezo sita, imeshindwa kupata ushindi kwenye nusu ya michezo hiyo halafu watu wanajadili uchawi...?

Ili uwe bingwa lazima uwe na mbinu za kimchezo zinazoweza kukupa matokeo. Haijalishi umechezaje mwisho wa siku kinachoangaliwa ni umepata nini.

Mpira bila magoli ni sawa na kumiliki simu kaliii halafu huna ubavu wa kuweka muda wa maongezi!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’