Makambo amepania kuwalaza na viatu Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
โ€ข
27 Sep 2018
Makambo amepania kuwalaza na viatu Simba
Ingawa mashabiki na hata viongozi wa Simba wanamchukulia poa Heritier Makambo kwa vile hofu yao kubwa ipo kwa Amissi Tambwe aliyerejea upya, lakini Mkon

Makambo anafahamu yeye na Meddie Kagere wa Simba ndio watakaokuwa wakitupiwa macho katika mechi ya watani hapo Jumapili, lakini amesisitiza anataka heshima kwa mashabiki wa Yanga na lazima aimalize Simba Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mchezo huo wa 101 kwa klabu hiyo tangu zianze kukutana katika Ligi 1965, Makambo alisema katika kitu ambacho atafurahi zaidi ni kuona anapata nafasi na kuifunga Simba kwani litakuwa jambo kubwa zaidi kwake.

Makambo alisema anajua amesajiliwa Yanga na nafasi yake anayocheza ni ya kufunga kwa kila mechi, hivyo hatafanya makosa Jumapili ili kuisaidia timu yake.

Alisema anafahamu Simba ni timu nzuri yenye mabeki wazuri wa kati kama Pascal Wawa na Erasto Nyoni, lakini amejianda kushindana kuipigania Yanga.

โ€œKambi tuliyopiga hapa Morogoro ni kwaajili ya kupata muda mzuri wa kutuliza akili na kuusubilia kwa umakini mchezo huo, hivyo naamini nitafanya vizuri Jumapili,โ€ alisema Makambo mwenye mabao mawili mpaka sasa.

Makambo alikosa mchezo uliopita wa Yanga na Singida United kutokana na majeruhi, hivyo Amissi Tambwe kupata nafasi ambayo Mrundi huyo aliitumia vyema vyema kwa kufunga mabao mawili, yaliyowapagawaisha Simba.

Simba wanaujua mziki wa Tambwe, ambaye msimu uliopita hakungโ€™ara kwa vile alikuwa majeruhi, lakini kurudi kwake upya na kutupia mabao mawili yamewapa presha mashabiki wa Msimbazi kuelekea mchezo wa Jumapili.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE โ†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE โ†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE โ†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE โ†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE โ†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE โ†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE โ†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE โ†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE โ†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE โ†’