Rekodi ya ushindi michezo minne mfululizo yaongeza mzuka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Sep 2018
Rekodi ya ushindi michezo minne mfululizo yaongeza mzuka Yanga
Mwezi huu wa tisa Yanga imeshinda michezo minne mfululizo, mitatu ikiwa ya ligi mmoja ukiwa mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon.

Aidha, Yanga imeanza ligi kwa kishindo baada ya kushinda michezo yake yote minne na kuifanya ishike nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 12 ikiwa imeshuka dimbani mara nne tu.

Yanga inakutana na Simba kwenye wakati muafaka kabisa. Ari na morali ya wachezaji iko juu kutokana na mwenendo wa timu.

Ushindi kwenye mchezo wa Jumapili utaifanya Yanga izidi kuitimulia vumbi Simba ambayo tayari iko nyuma kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Yanga huku ikiwa pia imecheza mchezo mmoja zaidi.

Yanga iko mkoani Morogoro ikiendelea kujifua na inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam keshokutwa Ijumaa, siku mbili kabla ya mchezo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’