Tambwe amkosha Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Sep 2018
Tambwe amkosha Zahera
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji Amissi Tambwe kwenye mchezo dhidi ya Singida United.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Taifa, Tambwe alifunga mabao yote mawili ya Yanga.

Zahera amesema kupitia mchezo huo amebaini kuwa Tambwe ni mmoja wa washambuliaji bora kwani hafanyi makosa anapopata nafasi langoni

Amesema Tambwe ana uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu na alidhihirisha hilo juzi kwa kufunga mabao kutoka nafasi mbili alizopata

"Tambwe ni mchezaji mzuri, anajua kukaa sehemu sahihi ya kufunga kama alivyofanya dhidi ya Singida United ni mabao ambayo hakuchezea nafasi alizozipata, hii inaonyesha namna alivyomakini kutambua majukumu yake anapokuwa uwanjani," amesema Zahera

Mchezo wa Jumapili Zahera atakuwa na uamuzi wa kutumia mshambuliaji mmoja au wawili baada ya kurejea kwa Tambwe huku Makambo nae akiwa amepona majeraha yake.

Majeraha yalimpoozesha Tambwe

Ni bahati mbaya kocha Mwinyi Zahera ametua Yanga wakati ambao Tambwe hakuwa kwenye kiwango bora kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu.

Msimu uliopita, Tambwe alikuwa nje karibu msimu na ilimlazimu kufanya kazi ya ziada kuweza kurejea dimbani kusakata kabumbu.

Rekodi yake ya kupachika mabao inamfanya awe mmoja wa washambuliaji bora kuwahi kutokea kwenye ligi ya Tanzania bara.

Sambamba na Makambo, anaweza kuibeba Yanga msimu huu kama hatayumbishwa na majeraha.

Tangu atue Tanzania msimu wa 2012/13 Tambwe amefunga mabao 68 kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara, akiibuka kuwa mfungaji bora misimu ya 2012/13 na 2015/16.

Ukiondoa msimu uliopita ambao majeraha yalimuweka nje, tangu atue Tanzania mwaka 2013, Tambwe amekuwa akifunga mabao zaidi ya 10 katika kila msimu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’