Baraza la Wadhamini, Kamati ya Utendaji Yanga wakutana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2018
Baraza la Wadhamini, Kamati ya Utendaji Yanga wakutana
Kabla ya usiku wa jana Jumatano Yanga kushuka uwanjani na kucheza na Coastal Union, Baraza la Wadhamini na kamati ya utendaji ya klabu hiyo walikutana ghafla na kujadili mambo mbalimbali, lakini kubwa likiwa ni Mwenyekiti wao, Yusuf Manji.

Wadhamini hao chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Kepteni George Mkuchika limekutana na Kamati ya Utendaji pamoja na kupongeza utendaji wao, lakini hoja ya Manji ilijadiliwa zaidi.

Taarifa zaidi ni kwamba baraza hilo, muda wowote linaweza kutoa tamko zito juu ya hatma ya uongozi wa klabu utakaotoa picha halisi ya hali ya uongozi ndani ya Yanga.

Mara baada ya kikao hicho hakuna mjumbe yeyote aliyeweza kuzungumzia kilichojadiliwa huku baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwasukumia baraza hilo kuongea.

"Tulikuwa na kikao na viongozi wetu ni kawaida kwetu kukutana, kilichojadiliwa ungewauliza wakubwa wetu ndio wenye mamlaka ya kuwaeleza haitakuwa busara tukiwasemea," alisema Hussein Nyika, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’