Kombe la FA kuanzia ngazi ya Wilaya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
Kombe la FA kuanzia ngazi ya Wilaya
Michuano ya kombe la FA (ASFC) inatarajiwa kuanza mwezi Oktoba ambapo kuanzia msimu huu mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia ngazi ya Wilaya.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi amesema wamepanua wigo wa mashindano hayo ili kuongeza ushindani.

Kulingana na Madadi, raundi ya kwanza itahusisha michezo ya kusaka mabingwa wa Wilaya baadae mikoa kisha timu hizo zitakazofuzu zitaunganishwa na timu kutoka ligi daraja la pili na la kwanza katika raundi ya pili.

Baadae raundi ya tatu itahusisha washindi wa raundi ya pili na timu za ligi kuu ya Tanzania Bara.

β€œTumeelekeza mashindano haya sasa yaanze kwenye ngazi ya Wilaya, tumewapa majukumu vyama vya mpira vya mikoa, kuhakikisha wilaya zinacheza kupata bingwa, na mikoa inacheza kumpata bingwa, kwa hiyo akipatikana bingwa wa mkoa, na mabingwa wa ligi ya mikoa, wale wataanza pale kwenye awamu ya mwanzo, awamu ya awali kushindana, kabla ya hatua ambazo zitaingiza timu za Daraja la Pili, la Kwanza na baadaye Ligi Kuu,” Madadi aliwaambia waandishi wa habari jana.

Mtibwa Sigar ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu uliopita na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika inayoanza mwezi Novemba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’