Leo kwenye mitandao ya kijamii habari inayojadiliwa zaidi ni kuhusu ratiba ya Yanga ambapo huenda ikapiga michezo 11 mfululizo kwenye uwanja wa Taifa.
Hata hivyo miongoni mwa michezo hiyo mingine Yanga itakuwa ugenini lakini itapigwa uwanja wa Taifa kutokana na timu inazochuana nazo kutokea jijini Dar es salaam.
Simba, JKT Tanzania, KMC na African Lyon zote ni za jijini Dar es salaam na zitatumia uwanja wa Taifa katika michezo yao ya nyumbani.

Kwa jinsi ratiba ilivyopangwa msimu huu imezingatia maeneo na umbali wa safari wa timu zinapokwenda kucheza mikoani.
Lakini pia swala la mapato linachangia kwa kiasi kikubwa kila timu kutaka kutumia uwanja wa Taifa hasa zinapopambana na Yanga na Simba.
Uamuzi wa kumfanya mwenyeji achukue mapato yote ya mlangoni tusishangae siku ikitokea timu nyingine za mikoa ya karibu na Dar zikahamishia michezo yao uwanja wa Taifa zitakapochuana na Yanga na Simba.
Yanga na Simba ndio timu zenye mashabiki wengi na michezo inayozihusisha timu hizo inayochezwa jijini Dar es salaam ndio inayoingiza fedha nyingi zaidi.

ADVERTISE HERE